Ufunuo wa Baha’u’llah unathibitisha kuwa kusudi la maisha yetu ni kumjua Mungu na kufikia uwepo Wake. Utambulisho wetu wa kweli ni roho yetu yenye mantiki, ambayo nia yake huru na uwezo wake wa kuelewa hutuwezesha daima kujiboresha wenyewe na jamii yetu. Kutembea katika njia ya utumishi kwa Mungu na jamii ya ya wanbadamu huyapa maisha maana na hutuandaa sisi kwa ule wakati ambapo roho huachana na mwili na kuendelea safari yake ya milele kuelekea kwa Muumba wake,

Hakuna kichoumbwa bila ajali yake maalum, kwani kila kiumbe analo daraja la asili la mafanikio … waalimu watukufu wanataka mwanadamu aelimishwe ili aweze kufikia ngazi ya juu kabisa ya uhalisi wake mwenyewe, ambayo kunyimwa kwake ni ngazi ya kupotea … mwanadamu anahitaji mwangaza wa Roho Mtakatifu … tunapokuja kwenye eneo la mwanadamu, tunakuta kuwa ufalme wake umevishwa ukuu mtukufu. Ukilinganisha na mnyama,ukamilifu na kasoro za mtu ni bora … hata hivyo ikiwa mtu ataridhika kuendelea kuwa katika hali ya kutokuendelea,akiangaliwa kutoka uwezo alionao, basdi yeye ni kiumbe wa chini kabisa. Ikiwa atafikia urithi wake kupitia hekima tukufu, hapo anakuwa kioo kilichotakata ambamo uzuri wa Mungu unaakisika; yeye anapata uhai wa milele na anakuwa mshiriki wa jua la ukweli. Hii inakuonesha jinsi vilivyo vingi viwango vya mafanikio ya wanadamu

Kusudi la mitume wa Mungu ni kumwinua mwanadamu kwa kiwango cha ujuzi wa uwezo uliomo ndani mwake na kumuangaza kupitia mwangaza wa ufalme, kubadilisha ujinga kuwa busara, utovu wa haki kuwa haki, kosa kuwa ujuzi, ukatili kuwa upendo na kutokuweza kuwa maendeleo. Kwa kifupi, kufanya mafanikio yote ya uwepo yangae ndani mwake.