Wa-Bahá'í wanajitahidi kujiweka sambamba na michakato inayojenga ambayo inahabarishwa na umoja huu wa kimsingi wa jamii ya wanadamu, dini, na Mungu, na kutembea pamoja juu ya njia ya utumishi.

WaBahá’í wanatoka matabaka yote ya jamii. Vijana na wazee, wanaume na wanawake kadhalika, wanaishi kando la wengine wa kila nchi na wanakuwa wa kila taifa. Wanashiriki lengo la pamoja la kuhudumia binadamu na kuboresha maisha yao ya ndani kufuatana na mafundisho ya Bahá’u’lláh. Jumuiya ambayo ni kwao ni moja ya kujifunza na kutenda, huru kutoka hisia yoyote ya kiburi au madai ya kuwa na uelewa wa pekee wa ukweli. Ni jumuiya inayojitahidi kukuza matumaini kwa wakati ujao wa binadamu, kuendeleza jitihada zenye madhumuni, na kusherehekea juhudi za wale wote ulimwenguni wanaofanya kazi kujenga umoja na kutuliza mateso ya kibinadamu.

Bahá’u’lláh aliwashauri wafuasi Wake: “Muwe wenye wasiwasi sana kuhusu mahitaji ya zama ambamo mnaishi, na mlengeni majadiliano yenu juu ya dharura zake na mahitaji.”