Wa-Bahá’í hulikataa wazo kuwa upo utata wa kiasili kati ya sayansi na dini. Badala yake wao wanaamini kuwa sayansi na dini ni taratibu mbili za ujuzi. Kila moja ikifanya kazi katika duara lake, kimsingi zimo katika upatano, zikiongezeana nguvu za kupeleka mbele ustaarabu

Imani inafundisha kwamba dini bila sayansi punde tu inaharibika na kuwa ushirikina na Imani kali; ambapo sayansi bila dini inakuwa chombo tu cha ulaji wa kawaida– na maendeleo ya kimwili yasiyo thibitiwa hayawezi kutupeleka kwenye ufanisi wa kweli.

Sayansi na dini vyote viwili vinaeleza uhalisi moja, na uhalisi ni mmoja. Haiwezekani kwamba kitu kikawa siyo sahihi kisayansi na kikawa cha kweli kidini. Mikanganyiko inatokana na mapungufu ya kiutu. Sayansi inazifunda akili zetu kugundua halisi zilizofichwa. Dini inatusaidia kugundua maana na matumizi sahahi ya uvumbuzi wa kisayansi.

Wa-Bahá’í wanaamini kuwa ni katika ufunuo wa Mungu peke yake wanadamu wanaweza kupata utaratibu wa thamani ambazo huyaweka maendeleo haya katika mtazamo linganifu. Dini inatoa majibu kwa yale maswali ya kimaadili, ya kusudi la kiutu, na uhusiano wetu na Mungu ambao sayansi haiwezi kuufikia. Katika wakati huohuo, Wa-Bahá’í wanaamini kuwa, dini yoyote inayopuuzia kweli za kisayansi za nyakati hizi yumo katika hatari ya kuingia katika msimamo mkali. Ni kwa kutambua asili ya upatano na ukamilisho wa sayansi na dini, hapo ndipo jamii ya kiutu inaweza kusogea mbele kwa usalama.

Kupitia misingi hii miwili ya sayansi na dini, tajiriba ya kiutu imepangiliwa, mazingira yake yametafsiriwa, nguvu zake zilizofichwa zimechunguzwa, na maisha ya kimaadili na kiakili yanapata nidhamu. Pamoja, wao wamekuwa wazazi wa kweli wa ustaarabu.